Umoja wa UIaya hautambui ushindi wa Maduro
5 Agosti 2024Kupitia taarifa yake, Stano ameeleza kuwa jaribio lolote la kuchelewesha uchapishaji wa matokeo ya kura litazidi kutia mashaka juu ya uaminifu wa matokeo yaliyochapishwa na tume ya uchaguzi.
Baada ya uchaguzi wa Julai 28, tume ya uchaguzi ya Venezuela ilimtangaza Rais Nicolas Maduro, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2013, kuwa mshindi.
Soma zaidi: Shinikizo kwa Nicolas Maduro lazidi kuongezeka
Hata hivyo, tume hiyo bado haijachapisha matokeo ya kura katika majimbo huku kukiwa na madai ya wizi wa kura.
Upinzani unaishtumu serikali kwa 'kuyachakachua' matokeo ya uchaguzi huo na unadai kuwa mgombea wake, Edmundo Gonzalez, ndiye mshindi halali.
Upinzani umesema umekusanya matokeo yao katika zaidi ya asilimia 80 ya majimbo nchini humo ambayo yanaonesha kuwa Gonzalez amepata asilimia 67 ya kura huku Maduro akipata asilimia 30 tu.