Umoja wa Ulaya waipatia Misri msaada wa dola bilioni 8
17 Machi 2024Jambo hilo linalohofiwa huenda likasababisha ongezeko la idadi ya wahamiaji watakaoingia barani Ulaya. Makubaliano hayo yamepangwa kusainiwa leo wakati wa ziara ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na viongozi wa mataifa ya Ubelgiji, Italia, Austria, Cyprus na Ugiriki.
Rais Abdel Fattah el-Sissi wa Misri amekutana kwa nyakati tofauti na von der Leyen pamoja na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo, ambaye nchi yake ndio kwa sasa inashikilia urais wa zamu wa Umoja wa Ulaya.
Soma pia: Umoja wa Ulaya kuimarisha uhusiano na Misri kwa kutoa ufadhili wa mabilioni dola
Mpango huo unalenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za nishati mbadala, biashara na usalama. Fedha hizo zitatolewa kama misaada, mikopo na ufadhili mwingine katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.