UN: Mataifa tajiri yalipe zaidi mabadiliko ya tabia nchi
14 Novemba 2024Matangazo
Ripoti hiyo itazinduliwa rasmi katika mkutano mkuu wa mazingira wa Umoja wa Mataifa COP29 huko Baku.
Uzinduzi huo utafanyika wakati ambapo viongozi wa dunia na wawakilishi wanatafuta kupata makubaliano mapya ya fedha.
Sudan yaongeza muda wa kukifungua kivuko cha Adre
Awali nchi tajiri duniani zilikuwa zimeahidi kutoa dola bilioni 100 kila mwaka kuzisaidia nchi zinazokuwa kiuchumi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, kama sehemu ya kutimiza yale yaliyokuwa katika makubaliano ya Paris.
Ila nchi zilikubaliana kwamba makubaliano mapya ya fedha hizo yanastahili kufikiwa kabla mwaka 2025.