UN na AU zahimiza amani kufuatia machafuko Senegal
3 Juni 2023Matangazo
Watu 9 waliuwawa siku ya Alhamisi baada ya kiongozi maarufu wa upinzani Ousmane Sonko kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili, kwa kosa la kuwachochea vijana, na huenda hilo likamuondoa katika azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2024.
Rais wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amewataka viongozi hao kuchukua hatua na kulinda demokrasia ya Senegal ambayo Afrika imekuwa ikijivunia. Nayo Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, imetoa wito kwa pande zote kulinda hadhi ya taifa hilo ya amani na udhabiti.