MigogoroSudan
UNHCR yahoji mustakabaliwa wa watu wa Sudan
23 Septemba 2024Matangazo
Filippo Grandi, Mkuu wa UNHCR amesema tangu kuanza kwa vita mwezi Aprili mwaka 2023, zaidi ya watu milioni 10 wa Sudan wamelazimishwa kuyahama makazi yao, wakiwemo milioni mbili walioondoka kabisa nchini humo na kuonya juu ya mizozo ya Afrika kusahaulika.
"Ni jambo la kutisha kusema kwamba kumekuwa na dhana, ambayo nadhani kwa bahati mbaya ni kweli, kuwa Afrika ina migogoro kila wakati. Sasa kumekuwa na aina ya mazoea, kuyachoka au kuyapuuza majanga hayo."
Grandi amesisitiza kuwa hali ya Sudan inatia wasiwasi pale watu wanapoanza kukimbilia mataifa yasio jirani akielezea ongezeko kubwa la Wasudan takriban 40,000 wanaowasili nchini Uganda na wengine karibu 100,000 wakiwasili nchini Libya.