UNICEF: Hali itakavyokuwa kwa watoto katika mwaka 2050
20 Novemba 2024Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatano ulimwengu unapoadhimisha Siku ya Mtoto Duniani, inatoa mitazamo tofauti, inayoonesha maendeleo katika afya na elimu ya mtoto, lakini pia inaibua wasiwasi kuhusu changamoto zinazotokana na hali ya hewa.
Watoto wanakabiliwa na maelfu ya migogoro
Katika taarifa ya kuashiria kutolewa kwa ripoti hiyo ya kila mwaka ya UNICEF, mkurugenzi wa shirika hilo Catherine Russell, amesema watoto wanakabiliwa na maelfu ya migogoro, kutoka kwa majanga ya hali ya hewa hadi hatari za mtandaoni, na kwamba hayo yote yanatarajiwa kuongezeka katika miaka ijayo.
Russell ameongeza kuwa miongo kadhaa ya maendeleo hasa kwa wasichana inakabiliwa na hatari.
Idadi ya vifo vya watoto itaendelea kupungua
UNICEF inasema kutokana na hatua za maendeleo zilizopigwa katika sekta za matibabu na teknolojia, idadi ya vifo vya watoto itaendelea kupungua.
Kufikia mwaka 2050, kiwango cha kuishi kwa watoto wachanga kinatarajiwa kufikia 98% na takriban 99.5% ya watoto wanaonusurika vifo wanapozaliwa, wanakadiriwa kuishi kwa zaidi ya umri wa miaka mitano.
UNICEF: Mamilioni ya wasichana wadhalilishwa kingono
Ripoti hiyo pia inaonyesha mafanikio makubwa katika elimu. Kufikia 2050, 96% ya watoto wanatarajiwa kumaliza angalau elimu ya msingi hili likiwa ongezeko kutoka 80% mwanzoni mwa karne.
Mwaka huu, UNICEF inatumia ripoti yake kutambua mitindo mitatu mikuu ambayo pamoja na migogoro isiyotabirika inaleta vitisho kwa watoto ikiwa watunga sera hawatafanya mabadiliko.
Hatari ya kwanza ni mabadiliko ya idadi ya watu, huku idadi ya watoto ikitarajiwa kubaki sawa na takwimu za sasa za bilioni 2.3, lakini watawakilisha sehemu ndogo ya idadi kubwa ya wazee duniani ya takriban bilioni 1.
UNICEF: Karibu watoto milioni 400 wananyanyasika kwa kisingizio cha kuwajenga kinidhamu majumbani
Katika baadhi ya nchi zilizoendelea, watoto wanaweza kuwa chini ya asilimia 10 ya idadi jumla ya watu ifikapo mwaka 2050, na hivyo kuibua wasiwasi kuhusu kuhusishwa kwao katika jamii pamoja na haki zao katika jamii zinazozingatia idadi ya watu wanaozeeka.
Tishio la pili ni mabadiliko ya tabianchi.
Mizozo yawazua mamilioni ya watoto afrika kushindwa kusoma
UNICEF inakadiria kuwa ikiwa mwelekeo wa sasa wa utoaji wa gesi chafuzi utaendelea, ifikapo mwaka 2050 watoto wanaweza kukabiliwa na mawimbi ya joto mara nane zaidi ya mwaka 2000, mafurikomakubwa mara tatu zaidi, na mara 1.7 zaidi ya mioto ya nyika.
Teknolojia mpya, haswa akili mnemba, ina uwezo wa kuleta uvumbuzi mpya na maendeleo lakini pia inaweza kusababisha ongezeko la ukosefu wa usawa uliopo kati ya nchi tajiri na maskini.
Hatma ya watoto imo mikononi mwa watunga sera
Naibu mkurugenzi wa kitengo cha utafiti cha UNICEF Cecile Aptel, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watoto wa siku zijazo wanakabiliwa na hatari nyingi, lakini kile walichotaka kubainisha ni kwamba suluhu ziko mikononi mwa watunga sera wa leo.