SiasaGeorgia
Upinzani nchini Georgia waitisha maandamano
28 Oktoba 2024Matangazo
Chama tawala kinachotuhumiwa kuegemea upande wa Urusi kimeshinda uchaguzi huo, ingawa Rais Salome Zurabishvili jana Jumapili aliituhumu Moscow kwa kuchochea udanganyifu kwenye uchaguzi huo.
Amesema kilichotokea ni operesheni maalum iliyoendeshwa na Urusi.
Kutokana na madai ya upinzani wenye hasira, Rais Zurabishvili na rais wa zamani aliyeko jela Mikheil Saakashvili wameitisha maandamano ya umma.
Umoja wa Ulaya ulionya kwamba uchaguzi uliofanyika unatazamwa kama mtihani wa kidemokrasia katika taifa hilo ambao huenda ukaamuwa uwezekano wa Tbilisi kujiunga na jumuiya hiyo.